latra tanzania
mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa nchi kavu (latra) ni mamlaka ya udhibiti wa serikali iliyoanzishwa kwa sheria ya bunge namba 3 ya mwaka 2019. sheria hiyo ni mbadala wa sheria ya zamani ya mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa nchi kavu na majini (sumatra). mamlaka imedhamiria kudhibiti sekta za usafiri wa nchi kavu hususan, usafirishaji wa mizigo na abiria (mabasi ya abiria, mabasi yaendayo kasi, mizigo ya kubeba magari, teksi, pikipiki na baisikeli), reli na usafiri wa kebo. latra ina ofisi yake kuu jijini dar es salaam, na ina ofisi za mikoa katika mikoa yote ishirini na sita (26) ya tanzania bara.
ADS